KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Friday, November 16, 2012

matanuzi nyumbani ugenini anakujua nani. Watoto wa Moïse Katumbi Chapwe, Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu waleta magari yao ya thamani Bongo.

Wachezaji nyota wawili wa timu ya taifa ya Tanzania na klabu ya Tout Puissant Mazembe TP Mazembe ya nchini Congo Mbwana Alli Samata na Thomas Ulimwengu jana wameingiza nchini Tanzania magari yao ya thamani waliokuwa wakiyatumia nchini Congo kwa ajili ya kuyatumia wanapokuwa hapa nchini.

Magari hayo ambayo waliyanunua wakiwa nchini Congo yameonekana kuwavutia watu wengi kutokana na kuonekana wake wa kisasa huku Samata akimiliki Chrysler Crossfire la mwaka 2006 ambalo linaarifiwa kuwa na thamani ya shilingi za kitanzania milioni 50 naye Ulimwengu akimiliki Benzi CLK 200.

Kwasasa wachezaji hao wako jijini Mwanza wakiwa katika kambi ya timu ya taifa ya Tanzania Bara inayojiandaa na michuano ya Challenge.
Rockersports ilifanikiwa kuyaona magari hayo yakiwa bado na namba za usajili wa Congo yakiwa yameegeshwa karibu na uwanja wa Taifa yakisafishwa ambapo dereva wa gari la Samata amesema kazi ya kuyatoa bandari ilikamilika jioni ya jana na hii leo wanakamilisha taratibu zote za TRA kabla ya kubadilisha plate namba ambapo amesema wachezaji hao wametaka usajili wa plate namba ufanywe wa majina yao.


No comments:

Post a Comment