KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, December 29, 2012

JUMA SEIF KIJIKO, SHAMTE ALLY, OBADIA MUNGUSA NA IBRAHIM JOB KUVAA JEZI YA AFRIKAN LYON MZUNGUKO WA PILI WA LIGI KUU TANZANIA BARA.

Kutoka kushoto, Juma Seif Kijiko, Obadia Mungusa, Shamte Ally na Ibrahim Job.
Wachezaji kiungo wa pembeni Shamte Ally, kiungo stadi wa kati Juma Seif Kijiko wa Yanga, mlinzi wa kati Obadia Mungusa wa Simba na mlinzi wa pembeni wa zamani wa Yanga Ibrahim Job, wanatarajiwa kuvaa jezi ya timu ya African Lyon ya Temeke jijini Dar es Salaam katika mzunguko wa pili wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara.

Wachezaji hao tayari wamekamilisha taratibu zote za kuhamia klabu hiyo katika kipindi cha dirisha dogo kwa mkopo, na tayari wameanza mazoezi na klabu hiyo katika uwanja wa Sigara ulioko Chang'ombe jijini Dar es Salaam.

Akiongea na Rockersports katibu wa Afrikan Lyon Brown Elias amesema uongozi wa Lyon umefurahishwa na ujio wa wachezaji hao ambao licha ya kwamba walikuwa hawapewi nafasi katika vikosi vya kwanza katika vilabu vyao lakini anaamini ni wazuri.

Amesema ni ngumu kupata nafasi katika vilabu vikubwa vya Simba na Yanga hata kama mchezaji ni mzuri kutokana na ushindani mkubwa wa kugombea namba miongoni mwa wachezaji na hiyo haiondoi uzuri wa mchezaji na kwamba kama mchezaji anajua kucheza basi atakuwa anajua tu jambo la msingi ni mazoezi na kujituma uwanjan.

Hata hivyo Brown amesema uongozi wa Lyon chini ya mkurugenzi wake Rahimu Zamunda Kangezi "mmachinga" umesikitishwa na kumkosa mshambuliaji mrefu kuliko wote katika ligi kuu ya soka Tanzania Bara Gaudience Mwaikimba kufuatia ombi lao kutolewa nje na uongozi wa klabu hiyo.

Lyon tayari imenza maandalizi ya mzunguko wa pili wa ligi kuu ya soka Tanzania Bara wakifanya mazoezi yao katika uwanja wa Sigara ulioko Changombe jijini Dar es Salaam. 

Kwasasa klabu hiyo haina kocha mkuu mara baada ya aliyekuwa kocha mkuu Pablo Ignacio Velez kutimka rasmi na sasa Afrikan Lyon inasaka kocha mrithi wake kabla ya kuanza kwa ligi kuu mzunguko wa pili.
Pichani Pablo Ignacio Velez kulia, alipokuwa akitambulishwa kwa waandishi wa habari mwezi Agosti. kushoto ni Rahim Kangezi na Charles Otieno katikati.

No comments:

Post a Comment