KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, December 15, 2012

VICTOR KOSTA NAMPOKA 'NYUMBA' AWASHANGAA MAKOCHA KWA KUMSUGULISHA BENCHI NA KUSAJILI WALINZI WA KIWANGO CHA CHINI KWA BEI MBAYA KULIKO YEYE. ANASEMA AGGREY MORIS, NADIR KANAVARO NA SHOMARI KAPOMBE WA KAWAIDA SANA TATIZO KUAMINIWA. ANASEMA HAONDOKI SIMBA MPAKA MKATABA WAKE UMALIZIKE.

 Mlinzi wa zamani wa kimataifa wa Tanzania ambaye kwasasa ana makataba na klabu ya Simba Victor Nampoka Kosta amelishangaa benchi la ufundi la klabu yake kwa kuendelea kumsugulisha benchi la timu hiyo.

Kosta pia ameshangazwa na usajili usiokwisha wa wachezaji wengine walinzi wa kati ambapo klabu hiyo imekuwa haishi kuchukua na kuwaancha wachezaji kibao katika eneo la ulinzi wa kati na yeye akiendelea kuonekana kama si lolote si chochote.

 Kosta ambaye kabla ya kurejea kwa mabingwa hao wa soka wa Tanzania Bara ambao sasa ni wawakilishi wa Tanzania katika michuano ya vilabu bingwa barani Afrika akitokea nchini Mozambique katika klabu ya Hidroelectrica de Cahora de Songo(HCB Songo), amesema yeye anajiamini kuwa bado anawezea kutoa mchango wake kwa kiwango cha juu ispokuwa ni suala la kuaminiwa na benchi la ufundi la timu yake.

Amesema anajuta kurejea nyumbani kucheza soka katika klabu hiyo ambayo wakati akiwa HCB Songo ya Mozambique uongozi wa Simba ulikuwa unamsumbua kwa kumpigia simu arejee kuichezea klabu hiyo jambo ambalo sasa linamgharimu kwa kuwa HCB Songo mpaka sasa bado inamhitaji.

Kosta amesema amechoshwa na benchi la Simba ambalo linazidi kumfanya aonekane kama mchezaji mstaafu wakati umri wake unamruhusu na uwezo wake bado ni mkubwa kuliko walinzi wa kati wengi wakiwemo walinzi wa kati wanaochezea timu ya taifa.

Ametolea mfano mchezaji kama Nadir Haroub ‘Kanavaro’, Aggrey Moris na Shomari Kapombe bila kutafuna maneno Victor Kosta ‘nyumba’ amesema wana uwezo wa kawaida sana lakini kwakuwa wana aminiwa na makocha na kupewa nafasi ndio maana wanaonekana wazuri ukilinganisha na wengine.

Amesema ameondoka Mozambique huku viongozi wa klabu yake ya HCB Songo wakisikitika na walikubali kwa shingo upande kwakuwa walimuamini sana katika ulinzi wa kati wa timu yao ilikuwa ikifanya vizuri katika ligi nchini humo, lakini mapenzi yake kwa Simba yalimfanya arejee nchini.

Ameishangaa kamati ya usajili ya Simba kwa kuendelea kufanya makosa ya kufanya usajili wa gharama kubwa kwa wachezaji wa kigeni wakati uwezo wao unafanana na wachezaji wa nyumbani ambao wana mapenzi na uchungu na vilabu vyao wanavyochezea.

Amesema mpira wa Mozambique uko juu ukilinganisha na Tanzania na kwenye ubora wa viwango wametuzidi hivyo haoni sababu ya kuhangaika wakati wao waliotoka nje walikuwa wanawaburuza wazawa wa nchi hizo ambazo ziko juu kisoka kuliko hapa.

Kosta amemtaja Obadia Mungusa kuwa ni mlinzi wa kati mzuri ambaye alikuwa akiichezea timu ngumu ya Mtibwa kabla ya kuhamia Simba ambako mpaka sasa anasugua benchi na uwezo wake kuiendelea kushuka.
Hata hivyo Victor Kosta alipoulizwa kama yuko tayari kupelekwa katika klabu nyingine kwa mkopo amesema hayukoa tayari kwa hilo na kwamba anasubiri mkataba wake na Simba umalizike ili akatafute maisha mengine ya soka sehemu nyingine.

“kaka siko tayari kwenda kokote kwa mkopo, nasubiri mkataba wangu na Simba umalizike nitafute mwelekeo, nashukuru nafanya mazoezi na wananilipa mshahara wangu”
“naipenda sana Simba, Kinacho nisikitisha hakuna mtu mwenye uamuzi wa mwisho, mara kocha, mara viongozi na mara mashabiki, kwa hiyo timu inayumba na wachezaji wanakufa moyo, lakini napenda sana kuitumikia Simba ndio maana nilikubali kurudi nchini”.

No comments:

Post a Comment