KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Saturday, September 21, 2013

BAADAYE KATIKA LIGI KUU YA SOKA TANZANIA BARA MAMBO YATAKUWA HIVI.

Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inaingia raundi yake ya tano jioni ya leo kwa mechi huku vinara Simba wakiwakaribisha Mbeya City kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Uwanja wa Mkwakwani, Tanga utakuwa mwenyeji wa mechi kati ya Mgambo Shooting Stars na Rhino Rangers ya Tabora. Mtibwa Sugar itakuwa mgeni wa Tanzania Prisons katika pambano litakalochezwa Uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine jijini Mbeya.

Nayo Kagera Sugar itakuwa nyumbani kwenye uwanja wake wa Kaitaba mjini Bukoba kuvaana na Ashanti United ya Dar es Salaam katika mechi itakayochezeshwa na mwamuzi Jacob Adongo kutoka Mara.

Ligi hiyo itakamilisha mzunguko wa tano kesho kwa mechi tatu ambapo Azam na Yanga zitacheza Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam huku JKT Ruvu ikikwaruzana na Oljoro JKT kwenye Uwanja wa Azam Complex.

Ruvu Shooting inayokamata nafasi ya pili kwenye msimamo wa ligi itakuwa mgeni wa Coastal Union katika mechi itakayopigwa kwenye Uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga.

Wakati huo huo, Ligi Daraja la Kwanza (FDL) inaendelea wikiendi hii kwa mechi kumi na moja. Kundi A hii leo kutakuwa na mechi kati ya Transit Camp na Green Warriors (Uwanja wa Karume, Dar es Salaam), Tessema na African Lyon (Uwanja wa Mabatini, Mlandizi).

Ndanda itacheza na Villa Squad kwenye Nangwanda Sijaona mjini Mtwara wakati kesho kutakuwa na mechi kati ya Polisi Dar es Salaam na Friends Rangers katika Uwanja wa Karume, Dar es Salaam.

Kundi B leo ni Mkamba Rangers dhidi ya Burkina Faso kwenye Uwanja wa CCM Mkamba, na Mlale JKT itakuwa mwenyeji wa Kurugenzi Mafinga kwenye Uwanja wa Majimaji mjini Songea. Keshokutwa (Septemba 22 mwaka huu) ni Majimaji na Kimondo katika Uwanja wa Majimaji.

Mechi za kundi C leo ni Pamba dhidi ya Polisi Dodoma (Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza), Stand United na Polisi Tabora (Uwanja wa Kambarage, Shinyanga) na Kanembwa JKT itacheza na Mwadui kwenye Uwanja wa Kawawa ulioko Ujiji. Kesho Polisi Mara na Toto Africans zitacheza Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume mjini Musoma.

No comments:

Post a Comment