KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, October 23, 2013

JAMALI MALINZI NA URAIS WA TFF HAYA NDIYO YA KWAKE NDANI YA TFF. Soma................




UCHAGUZI WA SHIRIKISHO LA MPIRA WA MIGUU TANZANIA (TFF) 2013ILANI YANGU YA UCHAGUZI

Utangulizi
Ndugu zangu,
Nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa Rehema aliyetulinda na kutuwezesha kufikahapa tulipo.

Tarehe 19 Novemba 2009 Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati anazindua ziara ya Kombe la FIFA la dunia uwanja wa Taifa, Dar Es Salaam pamoja na mambo mengine alisema, namnukuu:

‘‘Kwa Watanzania wenzangu tuichukulie ziara ya Kombe la Dunia nchini mwetukama ni changamoto kubwa kwetu inayotutaka tufanye vizuri zaidi katika soka ilitulingane na heshima hii tuliyopewa.

Hasa ni changamoto kwa viongozi wa soka wangazi zote pamoja na wachezaji na wapenzi wa mpira wa miguu nchini. Kuja kwakombe hili ni deni kwetu na kulilipa kwetu sisi ni kuzinduka, tuendeleze kiwangochetu cha soka nchini ili na sisi siku moja.

TUSHIRIKI FAINALI ZA
KOMBE HILI.

(Msisitizo ni wa kwangu). Hili jambo linawezekana. Wapo wenzetu Afrika wameweza, kwa nini sisi tusiweze? Wao ni watu kama sisi, maadam wameweza nasisi tutaweza.Lakini ili tuweze hatuna budi kuiga mfano hususani waliyofanya wenzetu na wanayoendelea kufanya kuendeleza mpira wa miguu.

Twende tukajifunze kutoka kwao. Lakini hata kabla ya kwenda huko, yapo mambo hatuna budi kuyafanya. Naomba nitaje baadhi yake:

1.Tuimarishe Uongozi, utendaji na uendeshaji wa vilabu vya mpira. Mchezaji hufundishwa kucheza mpira katika Klabu yake. Hapo ndipo hufundishwa maarifa ya kucheza mpira na vipaji kuendelezwa.

Hebu tujiulize hali ya vilabu vyetu vya soka ikoje. Je vinaongozwa vizuri? Vinaendeshwa vizuri? Jibu tunalijua sote kuwa ni hapana. Lazima suala hili tulitafakari kwa makinina kulipatia jawabu. Tukishindwa kupata jawabu muafaka na mambo yakaachwa kuendelea yalivyo, mpaka mwisho wa dunia hatutakuwa tunasogea popote.


2. Tupate walimu wenye uzoefu kufundisha timu zetu. Hii ndiyo njia ya uhakika ya kukuza na kuendeleza vipaji na hivyo kupata wachezaji bora.


3. Tuwekeze katika kuibua na kuendeleza vipaji vya wachezaji toka umri mdogo.Vilabu viwe na timu za watoto na vijana. TFF isaidie kuanzishwa kwa shule za mchezo wa mpira wa miguu kwa watoto na vijana. Mashuleni wapatikane walimu wa michezo walio wazuri kufundisha.

4. TFF ionekane zaidi ya ilivyo sasa katika mipango ya kuendeleza soka mashuleni, vijijini, mitaani na vilabuni. TFF ikiwa na mipango na kuisimamiana kuwabana wadau kuitekeleza itasaidia. Vinginevyo TFF itabakia kusimamia Ligi Kuu, kutoa adhabu kwa wachezaji na kusimamia timu yaTaifa. Hiyo haitoshi.’’
Mwisho wa kunukuu.

Ndugu zangu wajumbe wa Mkutano Mkuu wa TFF, wadau na wapenzi wa mpira wa Miguu Tanzania tujiulize kuanzia kipindi hicho cha 2009 hadi leo hii katika haya maagizo ya Mheshimiwa Rais JakayaMrisho Kikwete tumetekeleza yapi zaidi ya kuwa wasindikizaji katika medani ya kimataifa?

Kipindi chote cha miaka minane iliyopita Serikali imetoa sapoti kubwa katika sekta ya mpira wa miguu kwa kulipia walimu wa timu za Taifa na kuhimiza makampuni kama NMB, Serengeti Breweries, Airtel, CocaCola na sasa Tanzania Breweries kudhamini timu zetu za taifa na mashindano mbali mbali, matunda yake yako wapi? Ndo kwanza tunazidi kuporomoka kwenye viwango vya FIFA.

Iweje miaka ya nyuma timu zetu za Taifa zilifanya vizuri wakati zinaweka kambi Salvation Army, leo zinakaa hotel za nyota tatu mafanikio mbona hatuyaoni? 

Kama TFF imeondolewa gharama za kulipa makocha, kuweka timu kambini, kununua vifaa vya timu, dawa, posho, malazi pamoja na usafiri wa timu iweje leo TFF ishindwe kutumia vyanzo vyake vya mapato zikiwemo fedha toka FIFA na CAF kwa ajili yakuanzisha na kuendeleza programmu ya vijana ya kitaifa?

 Kwa mujibu wa mtandao wa FIFA kati ya mwaka 2008 na 2012 TFF imepokea toka FIFA msaada wa jumla ya dola za kimarekani milioni moja na lake nane na nusu (yapata shilingi bilioni tatu za kitanzania), hizi fedha zimefanyia nini?

 Kwa nini timu za vijana hazina udhamini? Ipi timu yetu ya taifa iwe ya wanaume wakubwa (senior team) ,wanawake au za vijana inayoweza leo hii kujivunia mafanikio? 

Iko wapi ligi ya wanawake? Katika hili tusilaumu Chama cha mpira cha wanawake, wakiwezeshwa wanaweza.Tutapataje timu mahiri yaTwiga stars bila ligi ya wanawake?

 Katika ngazi ya klabu, hasa zinazoendeshwa kwa mfumo wa kijamii kama Toto Africa, Coastal Union, Yanga, Simba, Mbeya City n.k. hadi leo hii pamoja na rasilimali za vilabu hivi ni klabu ipi imeweza kusimamia na kujiendesha yenyewe tokana na vyanzo vyake yenyewe? Tuendelee kujiuliza:

Ni walimu wangapi wa mpira tumewaendeleza kufikia kiwango cha kukabidhiwa majukumu yakufundisha Taifa Stars. Fursa za mafunzo tunazopewa na FIFA na CAF tunazitumiaje? Je tumeweza kuwa na angalau kocha mmoja anayefundisha mpira nje ya nchi kama ilivyo kwa akina Sam Timbe ( wa Uganda), James Sianga ( wa Kenya) Jack Chamangwana ( wa Malawi) na wengine ambao waliweza kufundisha mpira Tanzania kwa ufanisi?

Ni refa gani tumemuendeleza akafikia kiwango cha kuchezesha mashindano ya fainali za dunia au AFCON au Klabu bingwa ya Africa? Refa wa mwisho kuchezesha fainali za Mataifa Africa(AFCON) ni Omar Abdulkadir huko Burkina Faso mwaka 1998.

 Ni program ipi ya vijana ya kuibua vipaji na kuviendeleza tuliyo nayo? Wale vijana wa CopaCocacola 2007 waliopelekwa kwa mbwembwe Brazil waliishia wapi? Tuna rekodi zao? Tunajua wako wapi na wanafanya nini? Na hawa walioshinda majuzi Afrika Airtel Rising Stars tumewatangenezea program gani ya maendeleo?

Tunaelewa matatizo ya vilabu vya mpira hususani uhaba wa vifaa na pesa za uendeshaji, je vilabu vyetu TFF inavisaidiaje katika kuendeleza programu zao za vijana? Au kazi yetu ni kudai kila klabu iwe na timu ya under 20 bila kujali gharama za uendeshaji wa timu hizi?
 TFF hadi sasa imebuni, kusimamia na kutekeleza program endelevu ipi ya kuendeleza soka mashuleni, vijijini, mitaani au vilabuni? Au mpaka tusubiri Airtel rising Star na CopaCocacola? Siku wakubwa hawa wakisusa itakuwaje?

 Ziko wapi juhudi za kuhimiza upatikani wa vifaa vya kufundishia mpira watoto (kama mipira size 3/4) pamoja na kuimarisha miradi ya kuendeleza vijana ?

Hivi timu zetu za Taifa zinatumia mfumo upi wa uchezaji? Au kila kocha wa taifa tunayemleta anakuja na mfumo wake? Wenzetu wameweza kubuni mifumo ya uchezaji ya timu zao zaTaifa na wame ushirikisha katika mfumo wa ufundishaji wa watoto.
Lini Mwalimu wetu waTaifa alikaa na walimu wa vilabu (angalau vya Premier League) ili kujadili ufundishwaji wa mpira nchini, hii ikiwa ni pamoja na kujadili masuala yahusuyo mbinu, lishe, huduma za afyana ukakamavu wa mwili? Hivi mchezaji akitoka katika klabu yake ambako amezoea kula donana maharage ukampeleka kambi ya Timu ya Taifa akapewa prawns ,kuku na samaki kwa siku nne za kambi itamsaidia kumbadili siha? Ng’ombe hanenepeshwi siku ya mnada.Uratibu wa programu za vilabu ni muhimu.

Raha ya mpira ni kelele na hoi hoi za mashabiki. Wataalam wa mpira wanasema umoja wamashabiki wa mpira ni sawa na mchezaji wa 12 uwanjani. Zipo timu ambazo kihistoria zilikuwa ni za kijamii na zilihamasisha sana ligi ya Taifa, na kuiongeza hamasa na ushindani, Mbeya City ni mashahidi.

Leo hii ziko wapi timu kama Ushirika ya Moshi, Bandariya Mtwara, Kariakoo Lindi, Balimi Bukoba, Reli Kiboko ya vigogo, Kahama United, Mirambo ya Tabora, Tukuyu Stars, Nyota Korogwe, African Sports ya Tanga, Ujenzi Rukwa, MjiMpwapwa n.k. TFF imefanya juhudi gani kufufua ushidani huu kwa kushirikiana na vyamavya Mikoa na Wilaya?

Wapo wachezaji wastaafu waliojitolea kwa moyo mmoja kuiletea heshima nchi yetu. Leo hii tunasikia kina Alfonce Modest na Jellah Mtagwa wanalalamika hawana msaada, na hao ndio wale waliojitolea hadharani kutoa kilio chao. TFF hadi leo hii imewahi kuandaa mpango gani endelevu wa kuwasaidia wachezaji wastaafu? 

Shirikisho la mpira barani Afrika CAF wameanzisha ISSA HAYATOU TRUST FUND kusaidia wachezaji wastaafu waishio katika mazingira magumu, sisi tumechukua hatua gani katika hili?
 Iweje mpake leo hakuna mashindano yoyote ya wanawake ya kitaifa yawe ya ligi au yamtoano,angalau kwa ngazi ya kanda ? TFF itawezaje kuibua vipaji vipya vya timu ya taifa yawanawake TWIGA Stars bila mashindano ya aina hii?

 Vilabu vya mpira, hususani vya Ligi Kuu, vimegeuka kuwa kisima cha watu kuchota fedha. Haiyumkiniki vilabu ambavyo vinaweka timu kambini, kuihudumai kuanzia malazi, posho,vifaa, madawa na usafiri mwisho wa mechi jumla ya pesa wanayopewa inakuwa chini ya nusuya mapato yote ya mechi.

 Hayo maendeleo ya mpira ambayo yametakiwa yaanzie ngazi yavilabu yatapatikanaje? Vilabu vimegeuka vitega uchumi vya watu wengine wakati vyenyewe vinataabika na kujiendesha kwa mateso makubwa.
Ya kusema ni mengi, kwa leo tuishie hapa.

Nini matokeo ya hali hii? Takwimu hazidanganyi. Matokeo ya hali hii ni timu za Taifa kushuka viwango katika orodha ya FIFA siku hadi siku. Viwango vya timu za taifa vinapimwa kwa kuangalia uwiano wa matokeo ya timu ya wakubwa (senior) pamoja na yale ya timu nyingine za vijana za nchi husika.

 Miaka ya mwanzo ya tisini tulishawahi kupanda hadi nafasi ya 65, leo hii kila kukicha tuko kwenye 120.

Kuporomoka huku kutaendelea hadi lini? Ndugu zangu, tujiulize wapi tumetoka, tuko wapi na tunataka kuelekea wapi? Jibu ni rahisi, kamaalivyoagiza Mh Rais Kikwete,tujipange upya, tubuni mkakati wa uendelezaji wa mpira, tuandae program endelevu yenye malengo yanayopimika na kwa pamoja tukishirikiana na Serikali, FIFA, CAF na CECAFA, Halmashauri, Taasisi zisizo za kiserikali, Sekta binafsi, Vyombo vya habari na wadau wengine wote wa mpira wa miguu tutaweza kufanya vizuri na kuifanya Tanzania isifikeduniani kote. Katika kutimiza azma hii sharti tuanzie kwa kuleta.

mabadiliko
ya uongozi wa juu waTFF, tupate kiongozi ambaye sio sehemu ya mapungufu ya TFF, hakuna njia ya mkato.

Mimi Jamal Emil Malinzi, nimejipima na ninaamini nina uwezo wa kutosha wa kubuni, kuratibu nakusimamia mabadiliko haya nikiwa Rais wa TFF.

Ndugu zangu, siku zote si vyema kukosoa bila kueleza njia mbadala ya kufuata ili kutatua tatizo. Hapatunazungumzia mpira wa miguu na namna ya kuunasua toka kwenye janga la kushuka kiwango natimu zetu za Taifa kuendelea kugeuzwa kichwa cha mwenda wazimu ambacho hadi majuzi vibonde Gambia wamejifunzia kunyoa. Ili tuweze kuukwamua mpira wetu ni vyema tukakumbushana kuwa ili mpira uendelee unahitaji vituvinne:
1.Vipaji;
2.Walimu;
3.Vifaa;
4.Viwanja
1.Vipaji
Tanzania ni nchi yenye watu zaidi ya milioni 44. Nchi ya Cape Verde yenye watu 500,000 tuimeweza pamoja na uchache wake kuvumbua vijana 11 ambao wameweza kuifikisha nchi yao fainali za Africa 2013 Afrika Kusini na majuzi nusura waende kombe la dunia kama sio tatizo la utunzaji kumbukumbu. Sayansi ya uibuaji vipaji (scouting) ni muhimu na si kila mtuanaijua. Watafutwe wanaoijua, watufanyie kazi ya kutuibulia vipaji vipya, na katika hili nisharti mpira wa ushindani uchezwe nchini kote ili vipaji vionekane.

2.Walimu
Mpira ni sayansi,mpira ni taaluma. Kipaji bila mwalimu wa kukiendeleza ni bure. Vijanampira wanaanza kuucheza wakiwa wadogo hususani wakiwa shule za msingi. Huko ndikoTaifa linahitaji kusambaza walimu wenye taaluma ya kufundisha mpira ngazi ya awali.Wakishakuzwa kimpira ni lazima wawepo walimu wa kutosha kuwaendeleza ngazi yawakubwa na Taifa. Leo hii Uingereza ina walimu 1100 wenye leseni daraja A, Ujerumani wapo5500 na Hispania 12,000,Tanzania tunaye mmoja tu,kwa mtaji huu tutafika kweli?Kwa mujibuwa ripoti ya TFF nchi nzima ya Tanzania ina walimu wa mpira wa madaraja yote elfu mbili tuna mia tano kati yao wako Dar es salaam. Hawa walimu 2000 ndio wanategemewawawafundishe mpira vijana wa Kitanzania zaidi ya milioni kumi walio katika umri wakufundishwa mpira!

3.Vifaa
 Wachezaji, walimu wa mpira, madaktari na waamuzi wote wanahitaji vifaa vya msingi ilimpira uchezwe. Nchini mwetu vijana walio wengi wanacheza pekupeku, jezi ni upande mmoja kucheza kifua wazi, mpira ni wa kuviringisha matambara, refa anavaa suruali, filimbi ni mluzi, magoli hayana nyavu, n.k.

 Hii ndiyo hali halisi ya uchezwaji wa mpira maeneo mengi Tanzania hasa vijijini ambako ndiko kunapaswa kuwa chimbuko kubwa la vipaji. Gharama za vifaa vya michezo ziko juu mno, mfano mpira mzuri unaofaa kuchezewa kwenye ardhi ngumu (rough surface) bei yake ni shilingi laki tatu, shule ipi ya msingi itawezakuununua huu mpira?

 Kuna baadhi ya vyombo vya habari majuzi viliripoti kuwa kunamchezaji alifunga hat trick ngazi ya Ligi Taifa akanyimwa mpira kisa ni wa thamani kubwa. Mamlaka husika, hasa za kodi zinapaswa kuliangalia hili, ili upatikane unafuu katika bei zavifaa vya michezo maana karibia vyote vinaagizwa toka nje. Lakini pia vifaa vya michezo vyamisaada vinavyopatikana kutokana na miradi mbalimbali ya TFF ni juu ya TFF kuhakikishavinafikishwa vijijini pia kupitia vyama vya mikoa na wilaya.


4. Viwanja
Wilayani Ngara mkoani Kagera kuna uwanja wa mpira unaitwa ‘’Uwanja wa Changarawe’’ na ni kweli uwanja huo umejaa changarawe. Beki akikaba kwa mtindo wa kuteleza ardhini ‘sliding tackle’ basi nyama ya paja anaiacha pale chini. Hii ndiyo hali halisi ya viwanja vyetu vingi nchini, kama viponi vibovu sana maana maeneo mengi viwanja vya mpira hakuna vimechukuliwa na wajanja wachachena kugeuzwa makazi na majengo ya biashara. 
Tunahitaji viwanja vyenye ubora ili vijana wetuwafundishwe mpira wa kisasa kwa ufanisi, mpira wa kupiga pasi ya chini. TFF kwa kushirikiana navyama vya Mikoa na Wilaya sharti wawe mstari wa mbele katika kulipigania hili.

1.     TFF inatengeneza utaratibu mzuri wa kuuza bidhaa zake ndani na nje ya nchi kwa kupitia uuzaji wa kawaida na wa mtandao. Mikataba itaandaliwa ili kudhibiti uuzwaji holela wa bidhaa za TFF.

2.Vyumba vya Maduka vinajengwa kuzunguka uwanja wa Karume na kukodishwa.

3. Jengo la kitega cha uchumi litajengwa kwenye ardhi ya Uwanja wa Karume. Pia jukwaa la watazamaji litajengwa uwanja wa Karume ili mechi ambazo sio kubwa ziweze kufanyika pale, hii itaviongezea vilabu mapato.

4. Juhudi za kuboresha ukusanyaji, usimamizi na mgawanyo wa haki wa mapato ya milango ni yatokanayo na ligi yetu utaboreshwa ikiwa ni pamoja na kubuni vyanzo vipya kupitia njia mbali mbali zikiwemo za udhamini mbadala kwa vilabu. Aidha jitihada ambazo tayari zimekwisha anza za kuunda bodi ya kuendesha ligi na uanzishwaji wa utaratibu huru wakuendesha ligi zitaendelezwa ili kuongeza ufanisi, kuinua mapato ya vilabu na kuongeza msisimko wa ligi. Ninaunga mkono juhudi hizi.

5. Viwanja vingi vya mpira nchini vinamilikiwa aidha na Halmashauri, Serikali kuu au vyama vya siasa. Viwanja hivi vingi viko katika hali mbaya kuanzia nyasi ,hali ya uzio,vyumba vya kubadilishia nguo, mageti, vifaa vya kuzimia moto n.k. Ni vyema TFF na vyama vya mikoa kwa kupitia utaratibu wa PPP (Public Private Sector Partnership) vikaingia ubia na wamiliki wa viwanja hivi ili TFF nawashirika wake wachukue jukumu la kuviboresha, kuvisimamia na kuviendesha ilikuhakikisha vinakuwa katika viwango stahili kwa mujibu wa kanuni za FIFA naCAF. Hii itaongeza usalama wa wachezaji na watazamaji na kuinua mapatoyatokanayo na viwanja hivi

Ushiriki wa wadau Kwa sasa taswira ya mpira wa miguu inawafungia nje wadau wengi ambao kama wangepewa fursa ya kushiriki nao wangetaka wachangie maendeleo ya mpira wa miguu. Juhudi kubwa inabidi zitumike kurudisha imani hii ili kuleta hisia za umoja wa kitaifa katika kuendesha mpira wetu (sense of  belongingness) . Ni muhimu taasisi muhimu za kitaifa zishirikishwe katika sekta hii ya mpira wamiguu, hii ni pamoja na taasisi kama Tacaids,Mashirika ya utalii kama TANAPA na TTB, Umoja wa wafanyabiashara kama TPSF, CTI na TCCIA ,Kituo cha uwekezaji TIC n.k.Ushirikiano huu utasaidia kujenga jina la Tanzania pale tunapoandaa michuano ya kimataifa na pia kuhamasisha vijana wetu waepuke maisha hatarishi kama vile kujihusisha na ngono isiyokuwa salama,madawa ya kulewa(kutumia na kusafirisha), ulevi wa kupindukia n.k.


AHADI YANGU
Endapo nitachaguliwa kuwa Rais wa TFF, kwa kushirikiana na viongozi wote wa TFF kuanzia ngaziya vilabu, Wilaya, Mikoa na Kamati ya Utendaji Taifa na kwa kuhusisha kwa karibu Vyama vyakimataifa vya FIFA na CAF, Serikali, Halmashauri,Taasisi zisizo za kiserikali, Vyombo vya habari,Sekta binafsi, Mashirika ya umma na wadau wa mpira wa miguu Tanzania ninaahidi kuenzi mafanikioya awamu inayomaliza muda wake , kustawisha utulivu katika uendeshaji wa mpira, na kufanya jitihada za kubuni, kuboresha na kustawisha maendeleo ya mpira wa miguu Tanzania. Jitihada kubwazitawekwa kwenye maeneo makuu yafuatayo:

1.

Ufundi (Technical)
1.1 Muundo wa Idara ya UfundiKatiba ya TFF imeainisha wazi kuwa TFF ndiye msimamizi mkuu wa mpira wa miguuTanzania, hivyo jukumu la kuleta maendeleo ya mchezo huu kwa kiasi kikubwa linaiangukiaTFF.Ni kwa msingi huu basi asilimia kubwa ya rasilimali za TFF lazima iwekezwe katikakuleta maendeleo ya mpira. Kwa mfumo wetu wa uendeshaji, kichocheo kikuu cha maendeleoya mpira ni idara ya ufundi ya TFF. Hivyo idara hii ya ufundi inapaswa kuwa ndiyo idaramama ya TFF ambayo inapaswa kuongoza kwa matumizi ya fedha, idadi ya waajiriwa namatumizi ya rasilimali nyingine za TFF . Kwa sasa pale TFF hali sivyo ilivyo. Iwaponitachaguliwa nitapendekeza jukumu la kwanza la Kamati ya utendaji liwe ni kurekebisha nakuboresha mfumo wa uendeshaji wa idara ya ufundi. Nitapendekeza idara ya ufundi iendeleekuongozwa na Mkurugenzi wa Ufundi na chini yake awe na wakurugenzi wasaidizi wa vitengowatatu Mkurugenzi Msaidizi (ufundi), Mkurugenzi Msaidizi (Elimu na Mafunzo) ambaye kwasasa anaitwa Education officer, na Mkurugenzi Msaidizi (Maendeleo ya mpira).
Kitengo cha Ufundi kitahusika na kubuni na kusimamia shughuli zote zinazohusu maendeleo ya Timu za Taifa kuanzia za wakubwa hadi za vijana. Hii itakuwa ni pamoja na kuandaa mitaala ya taifa (national football curriculum) ya ufundishaji wa mpira Tanzania kuanzia umri wa miaka mitano hadi watu wazima.

   Walimu wa Timu za Taifa wataripoti kwake. Kitengo cha Elimu na Mafunzo kitahusika na kubuni na kuratibu kozi zote na mafunzo yoteyanayohusiana na mpira kama vile kozi za Marefa, Makocha, Madaktari, Makamisaa,Watawala, Waandishi wa Habari za Michezo, n.k.

Kitengo cha Maendeleo ya mpira kitahusika na kubuni,kuratibu na kusimamia mpango wamaendeleo ya vijana (grassroot) na kutafuta vipaji (scouting). Kitengo hiki kitafanya kazi kwa kushirikiana kwa ukaribu na idara za Serikali hasa idara za Elimu,Vijana na TAMISEMI,Halmashauri,Mashirika ya umma,Sekta binafsi pamoja na Taasisi nyingine za kijamii.

Wakuu wa vitengo hivi wataajiriwa kwa kufuata vigezo makini na bila upendeleo walakujuana.1.2

Ujenzi wa Kituo cha Mpira (Football Centre of excellency)Hiki ni Kituo Maalum cha mafunzo ya mpira wa miguu. Katika kituo hiki kunakuwa na kilaaina ya miundo mbinu, viwanja vya kufundishia mpira, vituo vya tiba,madarasa ,maabara zautafiti,hosteli n.k Kituo hiki pia kinakuwa ndio sehemu kuu ya kuweka kambi za timu za Taifana kutoa mafunzo ya ufundi yakiwemo ya ukocha, urefa, utawala na tiba.

 Wenzetu wa Senegal na Ethiopia kwa kushirikiana na Shirikisho la Mpira Africa CAF wameweza kujenga vituo hivi na matokeo yake tunayaona. Cameroon pia wana kituo hiki. Pamoja na gharama zake kuwa kubwa, cha muhimu hapa ni kuweka nia, kutafuta ardhi kwakushirikiana na Serikali na kuanza ujenzi taratibu. Kwa kuwa klabu ya Sunderland ya Uingereza na kampuni ya kufua umeme ya Symbion wameonyesha nia ya kushirikiana na Serikali kujenga kituo cha michezo itakuwa vyema iwapo TFF itashirikiana na taasisi hizi muhimu ili kufikia azma ya kujenga kituo hiki cha kisasa.

 Iwapo nitachaguliwa nitasimamia uanzishwaji wa mradihuu muhimu ikiwa ni sehemu ya mkakati wa kulikomboa soka letu.Aidha uwanja wa Karume yalipo makao makuu ya TFF utazungushiwa jukwaa ili mechiambazo sio kubwa zifanyike pale, Hii itaiongezea TFF mapato na vilabu pia.

1.3 Timu Kupanda Daraja Ili kuongeza ushindani na kupanua mpira uchezwe kona zote za nchini ( to spread the game), mtindo wa kucheza kikanda ili kupata timu za kupanda daraja kuu utakuwa ni wa kudumu na utaimarishwa kwa kutafutiwa udhamini na kuboreshwa viwanja kwa kushirikiana na wamiliki
wa viwanja hivyo.

 Usimamizi wa mashindano ngazi hii utaimarishwa na kusimamiwa kwakaribu zaidi ili timu itakayopanda daraja iwe imepanda kwa haki na hivyo kuleta ushindani Ligi Kuu.

Hata hivyo waraka uliotolewa na TFF ukiagiza mikoa ichezeshe ligi ili kupata bingwa wamkoa utafutwa kwa sababu hautekelezeki kutokana na hali ya uchumi na uhalisia wa jiografia ya mikoa ya Tanzania. 

Mathalani Mkoa wa Mtwara ukichezesha ligi ya mkoa (kwa maana yanyumbani na ugenini) ina maana bingwa wa Wilaya ya Masasi atasafiri vipi akacheze Newala au Mkoani Lindi bingwa wa Liwale atasafiri vipi akacheze na bingwa wa Kilwa, Pwani bingwa wa Mafia atasafiri kwa gharama za nani akacheze Bagamoyo na wa Kibahaakacheze Utete? Pamoja na nia njema ya TFF uhalisia hauruhusu.

 Kama Mwenyekiti wa chamacha mpira mkoa wa Kagera nalijua hili, hakuna haja ya TFF kuwa inatoa maelekezo ambayohayatekelezeki, hasa ukizingatia kuwa TFF hakuna msaada wanaopeleka kusaidia mikoa na wilaya ziandae mashindano yao. Vyama vya mikoa na wilaya viachwe viendelee kutumiaubunifu wao kupata mabingwa wao kulingana na hali halisi ya mazingira yao.

1.4 Kuanzisha mashindano mapya na kufufua ya zamaniWataalam wa kandanda wanasema kuwa ili mchezaji awe katika kiwango bora inabidi achezekwa mwaka kimashindano wastani wa mechi 40.
 Ligi yetu kuu,Vodacom premier league,inatoa fursa kwa mchezaji kucheza michezo 26 kwa mwaka iwapo anapangwa kilamechi.Hii haitoshi. Namna pekee ya kurekebisha hali hii ni kuongeza idadi ya mashindano kwamwaka.Hili litafanyika kwa kufufua kombe la Taifa (Taifa cup) na kuanzisha kombe lashirikisho (kama FA cup ya Uingereza). Kombe la shirikisho litashirikisha timu zote nchinikuanzia ngazi ya kata,tarafa,wilaya,mkoa hadi Taifa na bingwa wake atawakilisha nchi katikakombe la shirikisho la Afrika CAF confederation cup (kama ilivyo Kenya kwa sasa).
.5. Mpira wa WanawakeHadi sasa hatuna mfumo imara na unaoeleweka wa kuendeleza soka la kinamama. Mpira wawanawake umeanzia Wilaya ya Kinondoni, ukakulia Wilaya ya Kinondoni na umegoteaWilaya ya Kinondoni ambako kuna timu zenye majina kama Mburahati Queens na SayariQueens. Mpira wa wanawake sharti usambae nchi nzima, na ili kufanikisha azma hii lazimayaanzishwe mashindano ya kitaifa ya wanawake ikiwemo Ligi ya taifa ya wanawake. Hiiitaendana na juhudi za kuongeza makocha, waamuzi na makamisaa wanawake na kutafutaudhamini kwa timu ya Taifa ya wanawake TWIGA STARS.1.6 Maandalizi ya Vijana (Grassroot Programme)Mpango endelevu wa maendeleo ya soka la vijana sharti uandaliwe, uratibiwe na kusimamiwakwa makini. Program madhubuti ya maendeleo ya mpira wa vijana lazima ibuniwe ,iratibiwe

na kusimamiwa kwa usatadi mkubwa.Mradi huu lazima ulenge ,kwa hatua,kufikia hatua yakuingiza timu zetu fainali za kombe la Afrika la vijana chini ya umri wa miaka 17 na 20,fainaliza olimpiki, fainali za Afrika wachezaji wa ndani CHAN,fainali za Afrika AFCON na mwishofainali za kombe la dunia.Hii itakuwa ni pamoja na kujiwekea utaratibu wa mzuri wakuhakikisha vijana wetu wanapata fursa ya kucheza mpira nje ya nchi ili kujiongezeaumahiri.Na hii ni kwa wanawake na wanaume.Mpango huu ni lazima ushirikishe Serikali Kuu (hasa Wizara zenye dhamana ya Michezo,Elimu na Halmashauri), Taasisi zisizo za kiserikali,mashirika ya umma,sekta binafsi naTFF,CAF na FIFA. Ushirikishwaji wa Serikali na Halmashauri katika program hii ni muhimusana kwa kuwa ndio wasimamizi na wamiliki wa shule nyingi za msingi ambako ndiko vijanawetu wanakoanzia kucheza mpira. 

Mpango kazi huu lazima uonyeshe:

1.Nini tunataka kufanikisha.
2.Utaratibu utakaotumika.
3.Nguvu kazi inayotakiwa na sifa zake.
4.Mwongozo wa kufuatilia kupima ufanisi wa programu.
5.Kupambanua gharama za mpango na taratibu za uchangiaji wake.

Hatua muhimu katika kufanikisha program hii zitakuwa ni:-Kufundisha walimu wa walimu (instructors), hawa ndio watakuwa chachu ya kupatawalimu wa mpira mashuleni na mitaani.-Walimu wa walimu (instructors) kufundisha walimu wa kutosha wa michezo mashuleni namitaani-Kwa kushirikiana na wamiliki wa shule kuhakikisha viwanja vya kuchezea vinakidhiviwango-Kutafuta na kusambaza vifaa vya michezo mashuleni hasa mipira ya saizi muafaka kwamujibu wa viwango vya kimataifa.-Kupata shule angalau moja kila mkoa itakayopokea watoto wenye vipaji maalum vyakucheza mpira, pale ambapo wazazi hawataweza kuwalipia karo vijana hawa basi TFFihakikishe karo zao zinapatikana,huo ndio uwekezaji katika mpira.-Kuandaa mashindano mbali mbali yatakayoshirikisha shule hizi ili kupata timu za taifa zavijana wa umri mdogo wa kike na wa kiume.-Kuhakikisha timu hizi za umri mdogo zinapata fursa ya kushiriki mashindano mbali mbaliya kimataifa- Kupata vikosi vizuri vya timu za taifa za vijana wa umri mdogo ambao watakua pamoja,hao ndio watajenga msingi imara wa timu za Taifa za wakubwa kwa miaka ya baadae.Itakuwa ni muhimu sana program hii iendane vizuri na ratiba nyingine za mashindano yakitaifa kama Umitashumta, Umisseta, Airtel rising star, Copa Coca Cola n.k.


Kuanzisha mashindano ya kitaifa ya kombaini za shule za sekondari na ya kombaini zavyuo vikuu. Wachezaji mahiri wa timu ya taifa kama Leodeger Chilla Tenga (Rais waTFF) na Leopold Tasso Mkebezi (meneja wa Taifa stars) waliibukia kwenyemashindano kama haya Mkebezi akiwa beki wa kombaini ya sekondari zaBukoba,Ihungo,Kahororo na Nyakato.Aidha vituo vya michezo (sports academies) ambavyo tayari vipo vitatengenezewa utaratibuwa usajili na kuwekewa utaribu wa kuviendesha.Ili kuondoa ulalamishi wa vituo vya mafunzo (Academies) kulalamikia malipo pindi mchezajiakisajiliwa timu kubwa, vituo vyote vya vijana vitasajiliwa na vijana wao wote wataingizwakwenye kumbukumbu za TFF (data base) kwa majina, saini na picha,hii itasaidia kuzuia sakatakama la Mbwana Samata na klabu yake ya utotoni ya Mbagala maana kumbukumbu za TFFzitakuwa ndio jibu la maswali yote.
1.7
Tiba
1.

Tutaimarisha usalama uwanjani. Tutahimiza kila uwanja zinakochezwa mechi za ligi kuwe nagari la wagonjwa na chumba cha dharura (emergency room).Katika kuimarisha usalama tutahakikisha vifaa muhimu vya dharura kama vifaa vya hewa(oxygen) na vifaa vya kushtua moyo (defibulator) vinakuwepo. Kwa sasa hapa Tanzaniauwanja pekee wenye vifaa hivi ni Uwanja wa Azam Chamazi. Ni jambo la kusikitisha kuonahata uwanja mpya wa Taifa hauna chumba cha tiba dharura (emergency room) na kibaya zaidimakato ya uwanja hayaendi kuanzisha huduma hii muhimu wakati viongozi mbalimbali wakitaifa wanahudhuria mechi uwanjani.2.

Mradi wa Goal Project wa FIFA unatoa pesa za tiba na mradi huu uliweka lengo la kuwa nachumba cha kliniki pale uwanja wa Karume. Tutakifufua chumba hiki, tutakiwekea vifaa nakuhakikisha huduma ya kliniki kwa wanamichezo iliyokuwa ikitolewa na madaktari kilaJumapili inarudishwa. Posho itatafutwa ili madaktari watoa huduma angalau wapate nauli namaji ya kunywa.3.

Wakati wa kujadiliana mikataba na wadhamini mbalimbali tutahakikisha kipengele chahuduma za afya kinaingizwa katika mikataba. Udhamini utatafutwa kwa ajili ya vipimo vyawachezaji kabla ya league (pre-league medical test) kama vile vipimo vya uvumilivu (Yo-Yotest) na vipimo vya moyo (cardiac tests). Hii ni kwa ajili ya usalama wa wachezaji nawaamuzi.4.

Hadi leo chama cha Madaktari Tanzania, TASMA hakina ofisi. Hii ni aibu kwa chama chenyehadhi na umuhimu wa kipekee kama hiki. Tutahakikisha TASMA inapata ofisi yake pamojana chumba maalum cha kliniki.5.

Huduma ya afya lazima iwe sehemu maalum ya mfumo wa idara ya ufundi. Ni muhimu timuya madaktari wa Timu ya Taifa (National Medical team) ijulikane ni kina nani na wapewemikataba ya kazi. Hii tutalipigania.6.

Majeraha ya michezo huwa yanahitaji utaalam wake wa tiba. Tutaiomba Serikali itupeushirikiano ili kipatikane kitengo maalum cha kutibu majeraha ya wanamichezo (sports

injuries wing) katika baadhi ya hospitali zetu wakati tunajiandaa kuwa na kitengo cha tiba(Rehabilitation Centre) katika kituo cha michezo kitakachojengwa.7.

Ili kuimarisha uwezo wa madaktari wetu kutoa huduma za afya kwa wanamichezo,tutahakikisha madaktari wengi kadiri iwezekanavyo wanapata kozi za msingi,kati na juu(preliminary,intermediate and advanced). Nafasi hizi zitatolewa bila upendeleo wala kujuana.8.

Utoaji wa ushauri nasaha kwa wachezaji utaongezeka hasa kuhusu masuala ya ukimwi namadhara ya madawa ya kuongeza nguvu na ya kulevya.
.8
Waamuzi
Imepita miaka zaidi ya 15 toka Tanzania itoe mwamuzi wa kimataifa wa kuchezesha fainali kubwa(mara ya mwisho AFCON 1998), hii si sawa. Utaratibu uliopo sasa wa kuwapata na kuwaendelezawaamuzi ama una mapungufu au haufai kabisa hivyo budi utafutwe utaratibu ulio mzuri zaidi katikakupata waamuzi bora, tafiti zitafanywa ili kubaini ni njia zipi za kisayansi za kuwapata waamuzi bora(Top referees).Semina za mara kwa mara za CAF na FIFA ni nzuri lakini hazitoshi, TFF lazimaiwekeze kwa kutoa mafunzo zaidi ya waamuzi kwa gharama zake.Aidha mradi wa maendeleo ya mpira kwa vijana (grassroot) utahusisha pia mafunzo ya uamuzi wampira kwa vijana kama kinavyofanya kituo cha Jenerali Twalipo.Utaratibu wa kutoa adhabu kwa waamuzi wanaosemekana wameboronga uwanjani nao unahitajimarekebisho ya haraka sana. Uamuzi wa mpira ni taaluma kama zilivyo taaluma nyingine,mwamuziakikosea ni vyema akakosolewa na mwamuzi mwenzie ambaye ni mwandamizi,na kama nikuadhibiwa aadhibiwe na jopo la waamuzi wenzie waandamizi lakini wastaafu na sio mtu mwingineambaye hajawahi kupuliza filimbi.1.9
Makocha
Kumekuweko na utamaduni usiofaa katika soka la Tanzania miaka ya karibuni wa kuona kuwamakocha wa kigeni ndio bora zaidi na wanastahili mikataba,mishahara minono na marupurupuilhali makocha wazawa wanageuzwa ‘deiwaka’, jambo hili ni baya sana,ajira ziheshimiwe kwamsingi wa taaluma na sio kwa msingi wa nchi atokayo mtu.Makocha wetu wazalendo wana uwezo mkubwa kama wakipewa nyenzo kama wanazopatiwawageni, kama malipo mazuri, mikataba ya muda mrefu, vitendea kazi na kuheshimiwa programzao bila kuingiliwa na viongozi.Iwapo nitachaguliwa ninaahidi:- Kuwaendeleza makocha kimafunzo ndani na nje ya nchi kwa wale wenye uwezo nautashi wa kufanya hivyo.- Kushawishi taasisi za elimu nchini kama vyuo vikuu kufundisha taaluma ya ukocha- Kuhakikisha walimu wa mpira wa timu zetu za Taifa wanakuwa na mikataba stahiki, hiini pamoja na benchi zima la ufundi.

- Kuwajengea uwezo makocha wetu wazalendo ili nao wapate fursa ya kufundisha mpiranje ya nchi.- Kuanzisha tuzo za kila mwaka za makocha wazalendo ambao wamefanya vizuri katikaufundishaji wa soka la vijana la wanawake na wanaume.- Kuhakikisha utaratibu wa leseni za CAF unazingatia vigezo vya kitaaluma, uzoefu naushiriki wa kocha mhusika katika ufundishaji. Makocha ambao wanafundisha (activecoaches) watapewa kipaumbele katika kupata kozi za kupanda madaraja kuliko walewanaofungia vyeti makabatini.Leseni za CAF ni muhimu katika kumfanya mwalimu wampira atambulike kimataifa.- Kuhakikisha kanuni za ligi zinasimamiwa vyema ikiwemo kanuni itakayomlazimishakila mwalimu wa ligi kuu na daraja la kwanza awe mwanachama wa TAFCA (chamacha makocha nchini), walimu wa kigeni watapewa uanachama wa muda.1.10
Timu za Taifa
Timu zetu za Taifa, ziwe za wakubwa au za vijana ndio kioo cha mpira wa Tanzania. Jitihadazote lazima zifanyike kuhakikisha tunakuwa na timu nzuri za Taifa kuanzia za wakubwa(wanawake/wanaume) hadi za vijana. Pamoja na jitihada zitakazofanyika kuboresha idara yaufundi kama ilivyoanishwa hapo juu lakini pia yafuatayo ni mambo ya ziada yatakayofanyika.
(a)

Kuandaa fainali za Afrika za umri chini ya miaka 17 (U-17) mwaka 2019
Hadi sasa hakuna nchi ambayo imekwisha pata uenyeji wa mashindano haya. Uenyeji huuunatolewa na Shirikisho la vyama vya mpira Afrika CAF.Hii ni changamoto kwetuWatanzania kuomba uenyeji huu.Tukipewa fursa hii itatusaidia sana kutusukuma tuanzekuandaa programu ya nguvu ya miaka mitano ya kupata timu yetu itakayocheza katikafainali hizi kama wenyeji. Aidha kama nchi tutalazimika kuboresha miundo mbinu yetuhususani viwanja vyetu vya mpira, jambo ambalo litatusaidia siku za usoni. Ninaaminiuwezo wa kuandaa mashindano haya kama nchi tunao. Nikichaguliwa nitalisimamia hili.
(b)

Nidhamu
TFF itaandaa Kanuni za Nidhamu (code of ethics) kwa wachezaji, walimu na viongozi waTimu za Taifa mara wawapo ndani na nje ya uwanja. Hii itasaidia kujenga nidhamu yatimu. Kanuni hizi zitaendana sambamba na kanuni za maadili za TFF.
(c)

Walimu
Ni vyema siku za usoni timu zetu zote za Taifa zikafundishwa na makocha wazawa.Utaratibu utafanyika kuhakikisha makocha wasaidizi ambao ni wazawa wanaendelezwakufikia kiwango hicho, hii itakuwa ni pamoja na kuwapatia fursa za mafunzo ndani na njeya nchi.
d)

Zanzibar
TFF kwa kushirikiana na Chama cha Mpira Zanzibar ZFA tutahakikisha kunakuwa namahusiano ya karibu ya walimu wa timu za Taifa Zanzibar na Bara ili kuhakikisha timu bora ya Taifa inaundwa na vijana wa pande mbili za Muungano. Aidha jitahada za Zanzibar kuwa mwanachama kamili wa CAF na FIFA zitaendelea kuungwa mkono.
2.

Utawala
Inabidi tuendeleze utamaduni wa kuendesha shughuli za TFF kitaasisi (to have a corporateculture).Nguzo muhimu za uendeshaji shirikisho kitaaluma ni pamoja na kujenga nidhamu yawafanyakazi,heshima kwa uongozi,utunzaji wa kumbukumbu,ukarimu kwa wageni,umakinikatika manunuzi na utunzaji wa fedha pamoja na kufanya kazi kwa malengo na kuhakikishamalengo hayo yamefikiwa.
Maeneo yafuatayo yataboreshwa ili kuongeza ufanisi:
2.1 Ofisi za Mikoa na Vyama ShirikiKwa kuzingatia vyama vya Mikoa kuwa ndio muendelezo mkuu wa shughuli za TFF Mikoani,ni muhimu ofisi za mikoa zikawa kielelezo cha ufanisi wa utendaji wa TFF. Ofisi za Mikoazitaboreshwa hasa kwa kupewa vitendea kazi hususani vifaa vya mawasiliano.Vyama shiriki hadi sasa havina ofisi zenye hadhi ya vyama hivi, tutahakikisha tunaondoa aibuhii. Aidha kutokana na mapato ya TFF sehemu ya mapato haya itatengwa kwa ajili ya ruzukuya kupeleka kwenye vyama vya Mikoa na vyama shiriki ili isaidie kupunguza makali yakuendesha vyama vyetu.2.2

Ofisi ya RaisKutakuwa na ofisi ya Rais wa TFF. Ofisi ya Rais wa TFF (office of the President) lazimaiimarishwe na iwe sehemu itakayoweza kukabiliana na changamoto za maendeleo ya mpirawa miguu. Rais wa TFF ndiye msimamizi mkuu wa shughuli za mpira wa nchi hii,lazimaawe na mahali stahili pa kufanyia kazi kulingana na hadhi yake.Hii itakuwa ni pamoja nakuwa na wasaidizi wenye uweledi wa kutosha katika shughuli za kila siku za kuongozashirikisho.Ofisi za TFF makao makuu uwanja wa Karume zitakarabatiwa na kuongeza nafasi yakufanyia kazi.2.3 MaslahiMaslahi ya wafanyakazi wa TFF yataboreshwa ili kuwaongezea motisha. Hii itakuwa ni pamoja na kuwapa fursa ya kuhudhuria mafunzo mbalimbali.

2.4 Vilabu vya MpiraVilabu vitasaidiwa kupewa mwongozo wa kujiendesha kwa ufanisi zaidi. Aidha utaratibu wamgawanyo wa mapato ya milangoni utatazamwa upya kwa lengo la kuhakikisha vilabuvinapata mgao mkubwa kuliko iliyo sasa. Hii ni kwa kuzingatia gharama kubwa wanazoingiavilabu katika kuandaa timu ikiwemo malazi, usafiri, vifaa, posho, dawa, mishahara n.k.2.5 Wachezaji wastaafuHii ni hazina ya Taifa,kustaafu kwao kucheza mpira sio mwisho wao wa kuchangia maendeleoya mpira wa nchi yetu.Jitihada zitafanyika kuanzisha mfuko maalum (Trust Fund) ambaoutachangiwa na wachezaji wenyewe wanapokuwa bado dimbani pamoja na TFF, hii ni kwa ajiliya kuwasaidia hapo baadae wanapokuwa na matatizo hasa ya ugonjwa. Aidha chama chawachezaji wastaafu (SPUTANZA) kitapewa ofisi na kitaimarishwa ili kiwe kiungo muhimukati ya wachezaji na TFF.Wachezaji watahimizwa watumie chama hiki kutatua matatizo yao nachama kitapewa fursa kikanuni ya kuwa mtetezi mkuu na msimamizi wa maslahi ya wachezaji.

2.6 MikatabaUtaratibu wa TFF kuingia mikataba na wadhamini mbalimbali utarekebishwa ili kuongezauwazi. Ipo mikataba ambayo imesainiwa na TFF ambayo imesababisha vyama vya mikoa nawilaya, pamoja na uhaba wao wa pesa, wahangaike kutafuta fedha za zaida kuandaa timu zaokwa ajili ya mashindano yanayobeba jina la mdhamini kwa kuwa fedha anayotoa mdhaminihaikidhi uendeshaji wa mashindano yenyewe.Aidha vipengele tata vinavyokandamiza maslahi ya vilabu katika baadhi ya mikatabainayosainiwa kati ya TFF na wadhamini vitarekebishwa kama sio kuondolewa kabisa kwamaslahi ya ustawi wa mpira wetu. Haki za vilabu katika matangazo ya biashara yahusuyompira zitalindwa kwa nguvu zote.


1.

TFF inatengeneza utaratibu mzuri wa kuuza bidhaa zake ndani na nje ya nchi kwa kupitiauuzaji wa kawaida na wa mtandao.Mikataba itaandaliwa ili kudhibiti uuzwaji holela wa bidhaa za TFF.2.

Vyumba vya Maduka vinajengwa kuzunguka uwanja wa Karume na kukodishwa.3.

Jengo la kitega cha uchumi litajengwa kwenye ardhi ya Uwanja wa Karume.Pia jukwaa lawatazamaji litajengwa uwanja wa Karume ili mechi ambazo sio kubwa ziweze kufanyika pale, hii itaviongezea vilabu mapato.4.

Juhudi za kuboresha ukusanyaji, usimamizi na mgawanyo wa haki wa mapato ya milangoniyatokanayo na ligi yetu utaboreshwa ikiwa ni pamoja na kubuni vyanzo vipya kupitia njiambali mbali zikiwemo za udhamini mbadala kwa vilabu.Aidha jitihada ambazo tayarizimekwisha anza za kuunda bodi ya kuendesha ligi na uanzishwaji wa utaratibu huru wakuendesha ligi zitaendelezwa ili kuongeza ufanisi,kuinua mapato ya vilabu na kuongezamsisimko wa ligi.Ninaunga mkono juhudi hizi.
5.

Viwanja vingi vya mpira nchini vinamilikiwa aidha na Halmashauri,Serikali kuuau vyama vya siasa.Viwanja hivi vingi viko katika hali mbaya kuanzia nyasi ,haliya uzio,vyumba vya kubadilishia nguo,mageti,vifaa vya kuzimia moto n.k.nivyema TFF na vyama vya mikoa kwa kupitia utaratibu wa PPP (Public PrivateSector Partnership) vikaingia ubia na wamiliki wa viwanja hivi ili TFF nawashirika wake wachukue jukumu la kuviboresha,kuvisimamia na kuviendesha ilikuhakikisha vinakuwa katika viwango stahili kwa mujibu wa kanuni za FIFA naCAF.Hii itaongeza usalama wa wachezaji na watazamaji na kuinua mapatoyatokanayo na viwanja hivi

Ushiriki wa wadauKwa sasa taswira ya mpira wa miguu inawafungia nje wadau wengi ambao kama wangepewa fursaya kushiriki nao wangetaka wachangie maendeleo ya mpira wa miguu.Juhudi kubwa inabidi zitumikekurudisha imani hii ili kuleta hisia za umoja wa kitaifa katika kuendesha mpira wetu (sense of  belongingness) .Ni muhimu taasisi muhimu za kitaifa zishirikishwe katika sekta hii ya mpira wamiguu ,hii ni pamoja na taasisi kama Tacaids,Mashirika ya utalii kama TANAPA na TTB,Umoja wawafanyabiashara kama TPSF,CTI na TCCIA ,Kituo cha uwekezaji TIC n.k.Ushirikiano huu utasaidiakujenga jina la Tanzania pale tunapoandaa michuano ya kimataifa na pia kuhamasisha vijana wetuwaepuke maisha hatarishi kama vile kujihusisha na ngono isiyokuwa salama,madawa ya kulewa(kutumia na kusafirisha),ulevi wa kupindukia n.k.
http://htmlimg1.scribdassets.com/96xjz8waps30oagj/images/17-5622facc80.jpghttp://htmlimg1.scribdassets.com/96xjz8waps30oagj/images/17-5622facc80.jpg

HITIMISHO
Ndugu zangu,nihitimishe kwa kusisitiza kuwa maendeleo ya mpira Tanzania kwa hapayalipofikia yanahitaji ubunifu,ujasiri na msukumo mpya ili tuweze kuunyanyua mpira wetu nakuupa mwelekeo mpya,mwelekeo wa matumaini ,mwelekeo wa kulipeleka soka letu katikakushinda vikombe vikubwa barani mwetu Afrika na Duniani.Shime wapiga kura nipeni fursa hii ya kuwa Rais wa TFF ili kwa pamoja tukishirikiana nawadau wote muhimu katika sekta yetu tuweze kulisikuma gurudumu hili ili hatimae soka iwezekuiletea nchi yetu sifa na kuwapa raha mamilioni ya watanzania wapenda mpira.Pamoja tutawezaChagua MALINZIChagua MABADILIKOMungu ibariki AfrikaMungu ibariki TanzaniaJamal MalinziMgombea nafasi ya UraisTFF2013
Mpira ni afya, mpira ni burudani, mpira ni ajira kwa vijana!
http://htmlimg1.scribdassets.com/96xjz8waps30oagj/images/18-b62f3dc0a0.jpg


MAELEZO BINAFSI YA JAMAL EMIL MALINZI MGOMBEA URAIS TFFTarehe ya kuzaliwa
: 08 Agosti, 1960
Elimu
: 1974-1977 : Sekondari O-LevelMwanza Secondary School1978-1981 : A-LevelIlboru High School1980-1981 : JKT – RuvuOperesheni TIJA1981-1985 : Chuo Kikuu Dar Es SalaamDigrii ya Uhandisi (Upper 2
nd
Class)1986-1993

: Ajira -Coopers and Lybrand Tanzania Industrial Researchand Development Organization1993-Hadi Leo : MjasiriamaliMkurugenzi – Cargostars Limited
Michezo
: Nimekuwa promota wa mchezo wa ngumi za kulipwakuanzia kipindi cha 1995-2001. Baadhi ya mabondiawangu walifikia kiwango cha kimataifa hadi kusainimkataba na Promota maarufu duniani Don King.: Nimekuwa Seneta wa Yanga na baadae nikawaMkurugenzi na mwisho nikawa Katibu Mkuu wa Klabuya Yanga kati ya mwaka 1999 na 2005.: Nimekuwa Mkurugenzi na Msimamizi Mkuu wa Timu yaMkoa wa Dar Es Salaam ya Mzizima United. Timu hiindiyo ya mwisho kushinda Kombe la Taifa mwaka 2007ikiwa timu moja ya Mkoa wa Dar Es Salaam.: Nimekuwa mjumbe wa Baraza la michezo la mkoa waDar es salaam 2009-2011: Nimekuwa Mwenyekiti wa kamati ya mashindano mkoawa Pwani 2009-2011: Hadi sasa mimi ni mwenyekiti wa Chama cha mpira wamiguu mkoa wa Kagera: Kikampuni, Kampuni yetu ya Cargostars Limited inauzoefu wa muda mrefu wa kudhamini michezombalimbali. Kwa kipindi cha miaka saba CargostarsLimited iliidhamini mbio za marathon za wabunge.Aidha Cargostars Limited ina rekodi ya kudhaminimichezo mingine kadhaa ikiwemo mpira wa miguu, ngumi, Tennis na Golf.

No comments:

Post a Comment