KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Wednesday, December 18, 2013

KASI YA UFUNGAJI YA MANCHESTER CITY YATISHIA REKODI YA CHELSEA. Soma historia ya mabao kwa vilabu Ulaya......

Sergio Aguero (katika) na Alvaro Negredo (kushoto) wanaunganisha vizuri makali ya ufungaji ndani ya City Manchester

Ushindi wa Manchester City wa mabao 3-1 katika mchezo wa michuano ya Capital One dhidi ya Leicester umeifanya klabu hiyo yenye uwezo wa kufunga mabao ya mvua msimu huu kufikisha mabao 75 kutokana na michezo 25 ya michuano mbalimbali.

Namna ambavyo Sergio Aguero na Alvaro Negredo wamekuwa wakipishana kuandika mabao hayo wakichagizwa na msaada wa Edin Dzeko, Yaya Toure, David Silva na Samir Nasri kuiweka rekodi ya ufungaji wa mabao mengi inayoshikiliwa na Chelsea ya mabao mengi 103 katika ligi ya England Barclays Premier waliyoiweka msimu wa 2009/10 kuwa hatarini.
Ikiwa chini ya Carlo Ancelotti wakati ule, Chelsea ilifikisha jumla ya mabao 103 ambapo kwasasa, City imeshafikisha jumla ya mabao 47 katika jumla ya michezo 16.

Na wakati City inaovyoonekana ikitupa bunduki zao katika michuano ya vilabu Ulaya tayari inaonekana kuelekea kuvunja rekodi nyingine ya michuano hiyo kwa namna wanavyoonekana wakitupia nyavuni kiasi cha kutisha. 

 Historia inavyoonyesha

Real Madrid msimu wa 2011/12
Real Madrid iliweka rekodi ya kufunga jumla ya magoli 121 katika ligi huku Cristiano Ronaldo akifunga mabao 46 huku mengine 22 yakiwekwa wavuni na Gonzalo Higuain na mengine 21 yakifungwa na Karim Benzema.
Surly: But Real Madrid were remarkably consistent as they wrestled the Liga title from Barcelona in 2011/2012
Strength in depth: Gonzalo Higuain and Karim Benzema (right) were Real Madrid's strikers in 2011/2012
Strength in depth: Gonzalo Higuain and Karim Benzema (right) were Real Madrid's strikers in 2011/2012

 Gonzalo Higuain na Karim Benzema (kulia pichani juu) msimu wa 2011/2012

Barcelona 2011/12
Kikosi cha Pep Guardiola cha Barcelona wakati ule kilipoteza taji kwa wapinzani wao wakubwa Real huku Chelsea wakimaliza matumaini yao ya kutetea taji la mabingwa Ulaya katika hatua ya nusu fainali na kuelekea kushinda taji hilo.
Lakini bado Barca walimudu kufunga idadi kubwa ya mabao wakifunga mabao 190 msimu ule katika michuano yote naye Lionel Messi akiwa ndiye mfungaji wa msimu akitia kwenye kamba jumla ya mabao 73.
The greatest ever? Lionel Messi was the best player in one of the best teams in history
Embarrassment of riches: Andres Iniesta and Alexis Sanchez (right) were two more of Barca's attackers
Embarrassment of riches: Andres Iniesta and Alexis Sanchez (right) were two more of Barca's attackers


Chelsea 2009/2010
Msimu huu kurejea kwa Jose Mourinho ndani ya Chelsea kulipokelewa na mashabiki wa timu hiyo kama mwana mpotevu karejea (prodigal son coming home), lakini mafanikio ya msimu huo yalitokana na kazi nzuri ya aliyekuwa bosi wa muda kipindi hicho Carlo Ancelotti.

Kuelekea mafaniko ya kuweka rekodi ya mabao ya msimu huo ya mabao 103 katika ligi na kutwaa taji, Chelsea ilishinda idadi kubwa ya mabao dhidi ya Sunderland, Aston Villa, Stoke na  Wigan, kupitia kwa akina Frank Lampard na Didier Drogba na ambapo kila mmoja alifunga mabao 26 na 37.
Record breakers: Carlo Ancelotti's (left) Chelsea were the Premier League's highest scorers in 2009/10
Carlo Ancelotti (kushoto) akishangilia taji la Premier League na rekodi ya ufungaji msimu wa 2009/10
Cultured: Didier Drogba is among the best players in Chelsea's history, playing for them from 2004-2012
Didier Drogba ni miongoni kwa wachezaji wakubwa wa kihistoria wa Chelsea alifunga magoli 27 msimu wa 2009/10
Club favouirte: Frank Lampard is another, and scored an impressive 26 goals from midfield in 2009/2010
Frank Lampard ni mfungaji mwingine aliyechangia rekodi ya ufungaji ya klabu ya Chelsea msimu wa 2009/2010 akifunga mabao 26.



Aston Villa 1930/31
Licha ya kufunga mabao mengi 128 wakati huo ligi ikitambulika kama Division One, rekodi hiyo ya juu imeendelea kusimama hivyo mpaka leo. Villa ilimaliza ligi ya msimu huo katika nafasi ya pili nyuma ya waliokuwa mabingwa wa msimu huo Arsenal ambao wao aliweka nyavuni jumla ya mabao 127. Mkongwe wa Villa Tom ‘Pongo’ alitumbukiza wavuni mabao 50.
Bayern Munich 1971/72
Wafalme wa soka la Ujerumani ambao kwasasa ndio bora barani Ulaya wamekuwa wakisumbua Ulaya kwa miaka mingi. Wameendelea kuwa timu pekee nchini Ujerumani hususani katika ligi kuu ya nchi hiyo Bundersliga kupita idadi ya mabao 100 katika kampeni ya ligi hiyo ngumu barani Ulaya ambapo mwaka 1972 walifikisha jumla ya mabao 101 na kutwaa taji.

Gerd Muller alifunga jumla ya mabao 50 katika michuano yote na msimu uliofuata akafunga mabao 67.
Goalscoring great: Bayern Munich's Gerd Muller scored 50 goals in all competitions in 1971/1972
 Gerd Muller alifunga mabao 50 katika mashindano yote ya msimu wa 1971/1972
Ferencvaros 1948/49
Ulikuwa ni mwaka wa kumbukumbu kubwa kwa timu ya Ferencvaros ya Hungary ambayo ilishinda taji la ligi ya nchi hiyo mwaka huo maarufu kama 'Nemzeti Bajnoksag' kwa kufikisha jumla ya mabao 140 yaliyotokana na michezo 30.

Mfungaji wa mabao mengi alikuwa ni Ferenc Deak, ambaye alifumania nyavu mara 59 ambapo kabla ya msimu huo alifunga mabao 48 na mwaka wa nyuma yake alifunga jumla ya mabao 66.
Alizuiliwa kuelekea nje ya nchi tofauti na mwenzake wa nchi moja Ferenc Puskas, ambaye alionyesha mambo makubwa Ulaya.

Swali ni je nini angefanya mtu huyu endapo angepewa nafasi ya kujiunga na timu vigogo wa Ulaya.

No comments:

Post a Comment