KWA MAWASILIANO ZAIDI TUMIA BARUA PEPE rockersports212@yahoo.com AU TUPIGIE KUPITIA NAMBARI 0767166607 AU 0717166607. KARIBU SANA. 66666666607 AU 0717166607

Tuesday, November 4, 2014

Kocha wa Ajax Frank de Boer: tunawaheshimu na sio kuwaogopa Barcelona

Kocha wa Ajax Frank de Boer amesema kikosi chake kinapaswa kuwaheshimu na sio kuiogopa Barcelona"respect, but not fear" wakati wakijiandaa kukutana na wapinzani wao hao katika mchezo wa ligi ya mabingwa Ulaya katika dimba la Amsterdam ArenA hapo kesho Jumatano.
Wadachi hao walichapwa bao 3-1 katika mchezo wa mzunguko wa kwanza mwezi uliopita na De Boer anasema hawataweza kurudia tena mwanzo huo mbaya.
Akiongea katika mkutano waanahabari amesema 
"tunachopasw kufanya ni kucheza na kuwa na mpira wakati wote, tunapaswa kuwa makini zaidi tangu mwanzo wa mchezo kitu ambacho ni muhimu katika mchezo huo.
Huu utakuwa ni mchezo wa pili kwa Luis Suarez kuichezea Barcelona katika ligi ya mabingwa Ulaya atakapo kuwa dimbani Amsterdam ArenA Jumatano ya kesho kuvaana na Ajax katika mchezo wa kundi F.
Mshambuliaji huyo mwenye umri wa miaka 27 aliwahi kuichezea Ajax frontman kwa miaka mitatu na nusu kwa mafanikio kiasi kuwa mchezaji bora mara mbili wa Ajax kabla ya kuelekea Liverpool mwaka 2011

No comments:

Post a Comment